Re: Il ne faut pas s’attendre à un grand Mazembe face Simba
Posté : 04 mars 2011, 21:05
Le Coach Zambien"Patrick Phiri" de Simba FC donne son plan avant de croiser Yanga c Dimanche en Championat Local et le TP.Mazembe le 20 Mars a Lubumbashi...NB: Si tu ne comprend pas tuna
Yanga,Mazembe waifumua Simba
MICHAEL MOMBURI
KOCHA wa Simba, Patrick Phiri amebadili kabisa mfumo na kuufumua mtindo wa zamani na sasa ana staili mpya ya kuikabili Yanga na TP Mazembe.
Phiri amekuwa anafanya kazi kubwa ya kuwatengeneza wachezaji kisaikolojia akitazama zaidi mechi za Mtibwa, Yanga na TP Mazembe ambazo zimejipanga mfululizo kuanzia wikiendi hii.
Tangu Jumatatu iliyopita, Simba inafanya mazoezi makali kila alfajiri kuanzia saa 12:30 mpaka saa 2.30 asubuhi na hufanya pia jioni saa 10: 00 mpaka 12:30 yote ikiwa ni kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Phiri ameonekana akijaribu kuwa karibu zaidi na mchezaji mmoja mmoja pamoja na kuwafanyia vitu vya kuwajenga kiakili huku akikabiliwa na mechi hizo tatu ndani ya siku 20.
Katika siku za nyuma kabla ya mazoezi Phiri alikuwa akikusanyika na wachezaji wake na kuomba dua, lakini sasa huzungumza nao kwanza kwa takribani dakika 15 mpaka 20 halafu dua inafuata na mazoezi yanaanza na hali hiyo hufanyika kila asubuhi na jioni.
Katika kila baada ya dakika 45 mpaka saa moja huwaita tena wachezaji kujadiliana nao mambo ya kiufundi uwanjani huku wakijipooza kwa maji baridi, wakati mazoezi yakiendelea na amekuwa akionekana kuzungumza kwa karibu na mchezaji mmoja mmoja kumuelewesha mambo mbalimbali tofauti na baada ya mazoezi hukusanyika tena kwa pamoja kabla ya dua.
Ndani ya uwanja, Phiri amekuwa akisisitiza kumiliki mipira, kupiga pasi fupi za haraka, kujenga ukuta imara, umakini kwenye umaliziaji, kupiga krosi na kumalizia kwa kasi pamoja na kufunga mabao kwa vichwa mazoezi ambayo yanaonekana kuwasumbua wachezaji wengi isipokuwa Mbwana Samatta na Mussa Mgosi walioonyesha uhai.
Hata katika hoteli ya Lamada, Ilala ambako Simba imepiga kambi Phiri amekuwa na mazungumzo na wachezaji wote na mmoja mmoja mara kadhaa lengo ikiwa ni kuwaweka sawa kisaikolojia kwa michezo migumu inayowakabili hasa dhidi ya Yanga Machi 5 na dhidi ya TP Mazembe kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika Machi 20 jijini Lubumbashi.
Phiri alisema mazoezini kuwa; "Tuna mechi ngumu sana inabidi tuwe karibu sana na wachezaji ili kuwaweka vizuri kisaikolojia na kila mmoja aelewe umuhimu wake na nini kinatukabili."
"Muhimu ni kwamba tupo kambini pamoja, hii inasaidia sana, hata katika mazoezi umeona nazungumza nao sana kwavile wakati wa mechi muda unakuwa mfupi, kumbuka tuna mechi ya Mtibwa Jumapili, inafuata Yanga baadaye AFC halafu ngumu zaidi ya Mazembe ugenini kwahiyo inabidi kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja ili kufukia upungufu tulionao.
"Inabidi wawe na mbinu mbadala za kufunga mabao, hizo mechi zimebanana sana ndio maana unaona tunakazana na kuwa na programu nyingi.
Viongozi mbalimbali wa Simba, akiwemo Makamu Mwenyekiti Godfrey Nyange 'Kaburu' wamekuwa sambamba na wachezaji kuanzia kambini mpaka mazoezini na Kaburu aliiambia Mwanaspoti kuwa; "Vijana wako vizuri na mazoezi yanakwenda sawasawa tunajaribu kufanya kila kinachowezekana mambo yaende vizuri."
http://www.mwanaspoti.co.tz/wcreadnews.php?id=6095